Bakuli latembezwa na Chadema kuwakabili kina Mdee

HomeKitaifa

Bakuli latembezwa na Chadema kuwakabili kina Mdee

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeanza kuchangisha fedha kutoka kwa wanachama wake, kugharamia mawakili watakaosimamia kesi ya waliokuwa wanachama wa chama hicho Hakima Mdee na wenzake 18 waliofungua shauri la kupinga kuvuliwa uanachama.

Akizungumza na Mwananchi jana, Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Mhusiano wa Chadema, John Mrema alisema chama hicho kimeipa Baraza la Wanawake (Bawacha) kusimamia michango hiyo.

Mrema alisema uamuzi wa kuchangisha fedha kugharamia mawakili katika kesi zinazokihusu chama hicho umekuwa ukifanyika, akitolea mfano wakati wa kesi ya Mwenyekiti Freeman Mbowe.

 

error: Content is protected !!