Ashtakiwa kwa kununua Premio badala ya tani 60 za mahindi

HomeKitaifa

Ashtakiwa kwa kununua Premio badala ya tani 60 za mahindi

Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa limemkamata Castory Mapunda (42) anayetuhumiwa kutumia sehemu ya Sh milioni 41 alizopewa kwa ajili ya kununua mahindi tani 60, kujinunulia gari ya kutembelea aina ya Toyota Premio.

Akizungumza na wanahabari jana Septemba 19,2022, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi alisema mtuhumiwa huyo mkazi wa Songea mkoani Ruvuma alipewa kiasi hicho cha fedha na Sadiki Kikoti (45) mkazi wa Kibwawa, mjini Iringa.

Katika tukio hilo lililotokea hivi karibuni, Kamanda Bukumbi alisema mtuhumiwa huyo alifanya wizi huo wa kuaminiwa baada ya kupokea kiasi hicho cha fedha kupitia akaunti namba yake 0152677424700 ya CRDB benki kutoka kwa mlalamikaji huyo.

“Alitumiwa fedha hizo ili amsaidie Kikoti kununua kiasi hicho cha mahindi. Hata hivyo mtuhumiwa alitoweka na fedha hizo na baada ya kukamatwa na kupekuliwa alikutwa na gari hiyo namba T 269 EAC na alipohijiwa alikiri kuinunua kwa Sh milioni 18 ambazo ni sehemu ya fedha hizo,” alisema.

error: Content is protected !!