DK. Kikwete achaguliwa kuongoza uchaguzi Kenya

HomeKimataifa

DK. Kikwete achaguliwa kuongoza uchaguzi Kenya

Rais wa awamu ya nne wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ameteuliwa kuongoza ujumbe wa Wachunguzi wa Uchaguzi Mkuu wa Kenya kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Ujumbe huo wa Maafisa 52 utakuwa ukiangazia kiwango cha matayarisho na mchakato mzima wa Uchaguzi Mkuu wa Kenya unaotarajiwa kufanyika August 09,2022 na baadaye Maafisa hao watatoa ripori Agosti 11,2022.

Dk. Kikwete amesema kwamba ujumbe huo ni kwa ajili ya kuhakikisha kuna maandalizi mazuri na Uchanguzi ufanyike kwa amani pia kutoa ushauri wa namna bora ya kufanya uchaguzi kwa hali ya utulivu.

error: Content is protected !!