Diamond kushindwa kuseme umri wake kwa kiingereza ni kosa?
Msanii mkubwa na mmiliki wa lebo ya WCB, Diamond Platnumz siku za hivi karibuni amezungumziwa sana mitandaoni baada ya kushindwa kutaja umri wake kwa usahihi kwa lugha ya kiingereza.
Katika ‘series’ iliyoachiwa Machi 18 Netflix Mondi alisema “I am thirty first” badala ya “I am thirty one” msemo ulioibua mijadala mitandaoni juu ya ujuzi wake wa kuongea lugha hiyo ya kigeni.
Wengi walijitokeza kukejeli “broken english” ya mwanamuziki huyo katika series hiyo huku wengine wakishangaa kwanini Diamond achekwe kwa kukosea lugha ambayo si yake ilihali angeweza kujieleza vizuri zaidi kwa Kiswahili.
“Licha ya Kiingereza chake kibovu (kulingana na wewe) Diamond alinifundisha kitu kimoja, kuwa mwanaume wa kiwango. Kwenye series anajaribu kiwango cha juu kuwa Simba mwituni/kuwa mfalme wa ‘show’. Mbali na yote series ni kati yake na
@ZariTheBosslady #VijanaMaarufuMwafrika.” ameandika mwanatwitter.
Despite of his broken English (according to you) diamond taught me one thing, to always be the man of the show. In this show he is trying his level best to be the lion in the jungle/to be the king of the show. After all the show is btn him and @ZariTheBosslady #YoungFamousAfrican pic.twitter.com/wupJrnHs9N
— Matendo (@HusseinActions) March 19, 2022
“Watu wanaocheka kiingereza cha Diamond wanajikanganya. Huyu mtu ametoka kwenye maisha duni hadi kuwa msanii anayeongoza Afrika na unaangalia zaidi Kiingereza chake. Lugha ya wakoloni?” Aliandika mmoja wa wafuasi wa Twitter.
People laughing at Diamond’s English is baffling. Like this man really came from nothing to being Africa’s leading artist and you’re concentrating on his English. The colonizer language? #YoungFamousAfrican
— Pretty Privileged ? (@muslamicchai) March 19, 2022
Washiriki wote katika ‘series’ hii ni Waafrika ambao mara chache walikuwa wakizungumza maneno machache kwa kilugha lakini kwa upande wa Diamond alijivunia lugha yake na kujitahidi kuzungumza sentensi kadhaa za Kiswahili katika baadhi ya sehemu alipokuwa akijielezea kwani Kiswahili ndiyo lugha ambayo ameibobea zaidi na kwa nafasi aliyonayo kwenye jamii basi amekipaiza Kiswahili.
Zari ambaye ni mama watoto wa Diamond naye ameonekana kwenye ‘series’ hiyo kama mwanamke jasiri na mwenye kujiamini na kila alipoingia alionekana kujua nafasi yake bila kutetereka.
Ni sawa kuwahukumu Waafrika kwa kushindwa kuzungumza lugha za kigeni? Unadhani Netflix walikosea kuiacha sehemu hiyo yenye kosa? Nani amekuvutia zaidi kwenye series hii?