Mdee: Sikutegemea haya ndani ya Chadema

HomeKitaifa

Mdee: Sikutegemea haya ndani ya Chadema

Baada ya Baraza Kuu la Chama cha Demokrasia na Maendeleo kukaa na Kamati Kuu kuridhia uamuzi uliotolewa na wajumbe kuhusu kuwafukuza wanachama 19, mmoja wa wanachama hao, Halima Mdee amedai kwamba mchakati mzima wa upigaji kura za maoni ulifanyika kihuni na kusema kwamba hata Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe anatambua ukweli huo.

“Kilichotokea pale naweza kusema ni uhuni, unajua mimi nimekua nipo kimya kwa muda mrefu sana na nitaongea siku nyingine, leo sio wakati muafaka, lakini wajumbe wa baraza kuu hata nyie mngekuwepo huko ndani kilichofanyika na mimi nakuwaga nakwepa sana kuzungumza maneno makali kwa sababu na heshimu sana viongozi wangu lakini sikujua kama Chadema unaweza ukafanyika uhuni wa kiwango hiki,

“Mimi ni Chadema, naendelea kuwa Chadema vizuri tu lakini kilichofanyika pale my friend ni uhuni wa kiwango cha hatari…situko chini ya jua na tuna muamini Mungu mmoja sio, kilichofanyika pale hata Mbowe mwenye anajua ni uhuni,” alisema Halima Mdee.

Akizungumza kuhusu kauli hiyo ya Halima Mdee, Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe amesema kwamba maamuzi yamefanyika hadharani na sio kama wananchama hao wanavyodai.

“Maamuzi ya kuwafukuza yalifanyika tangu mwaka juzi kwenye kikao cha Kamati Kuu, tangu mwaka juzi hakijakaa kikao cha Baraza Kuu, Baraza Kuu limekaa kikao leo na wao walikuwa mashuhuda na wameona maamuzi ya wajumbe. Sasa wakilalamika maamuzi yalifanyika kabla yalifanyika na wajumbe walikuwa wapi hao wajumbe, wajumbe wamekuja leo na mkutano umekaa jana wamefanya maamuzi wakiona, sasa wanataka kusema maamuzi yamefanyika jana na nani na kura zimepigwa mbele yao waache mambo ya kihuni,” alisema Mbowe.

Katika kupiga kura za maoni idadi ya wajumbe 423 walikubali uamuzi wa kuwafukuza uanachama sawa na asilimia 97.6% , Wasiokubali ni 5 sawa na asilimia 1.2% na wasiofungamana upande wowote ni 5 sawa na asilimia 1.2%.

error: Content is protected !!