Waliogushi barua warudhiswa kazini

HomeKitaifa

Waliogushi barua warudhiswa kazini

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa amemuagiza Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia TAMISEMI Ndg. Ramadhani Kailima kuwafuatilia watumishi 12 Mkoani Tanga waliogushi barua za Uhamisho na haraka sana warudishwe kwenye vituo vyao vya Kazi.

Mhe. Bashungwa ameongeza kuwa watumishi hao 12 wachukuliwe hatua stahiki za kinidhamu kwa suala la kugushi nyaraka za Serikali.

“Naagiza wote wote waliofanya hivyo watambuliwe kisha Katibu Tawala wa Mkoa awape barua za kuwataka kwa kipindi cha siku tano wawe wamerejea vituo vyao halali kwa gharama zao na iwapo walilipwa pesa za kujikumu (per diem allowance) na usumbufu (disturbance allowance) zilizotokana na uhamisho huo wa kugushi, waelekezwe kuzirejesha ndani ya kipindi cha miezi miwili ya Mei na Juni, 2022”

“Mamlaka za nidhamu kwenye Halmashauri zao zielekwezwe kuwachukulia hatua za kinidhamu kwa kosa la kugushi, kuitia hasara Serikali kwa kujipatia fedha (posho ya kujikimu na usumbufu) isivyo halali, kuufanya utumishi wa umma kudharaulika, kwenda kinyume cha maadili ya utumishi wa umma n.k na pia Mamlaka za Usalama, Polisi na PCCB ziwahoji ili wamtaje aliyegushi saini ili kupata mtandao mzima” amesema Waziri Bashungwa.

Waziri Bashungwa ametoa agizo hilo wakati wa Kikao na Waandishi wa habari kuhusu Matokeo ya Taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha 2020/21

error: Content is protected !!