Dkt. Mpango na safari ya Uswisi

HomeKimataifa

Dkt. Mpango na safari ya Uswisi

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango leo tarehe 20 Mei 2022 anatarajiwa kuondoka nchini kuelekea Davos nchini Uswisi ambapo atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani (World Economic Forum) unaotarajiwa kufanyika tarehe 22 hadi tarehe 26 Mei 2022.

Katika mkutano huo, Makamu wa Rais atahudhuria mikutano mbalimbali inayohusu masuala ya biashara na uwekezaji, ulinzi na usalama, usalama wa chakula, mazingira pamoja na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani unahudhuriwa na Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa mbalimbali, Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa, Wakuu wa Taasisi na Makampuni mbalimbali duniani pamoja na Wafanyabiashara.

error: Content is protected !!