Watangazaji walazimika kuficha sura

HomeKimataifa

Watangazaji walazimika kuficha sura

Sheria mpya ya viongozi wa Taliban nchini Afghanistan imewalazimisha waandishi wa habari na watangazaji wanawake kuziba nyuso zao wanapoonekana kwenye runinga.

Awali sheria hiy haikutilia maanani sana lakini kuanzia jumapili ya jana watangazaji wamelazimishwa na wakuu wao wa kazi kufuata utaratibu huo kama ambavyo nao wamepokea maagizo hayo kutoka kwa viongozi wengine wa ngazi za juu yao.

Wizara ya Habari na Utamaduni hapo awali ilitangaza kuwa uamuzi huo ni hatua ya mwisho na “haitojadiliwa.”

Baadhi ya watangazaji wanawake wamejitokeza na kupinga vikali uamuzi uluofanywa na Taliban. “Ni utamaduni wa nje tuliowekewa, unaotulazimisha kuvaa barakoa, na hilo linaweza kutuletea tatizo wakati wa kuwasilisha vipindi vyetu,” alisema Sonia Niazi, mtangazaji wa habari katika kituo cha TOLO.

“Amri hii haitabiriki kwa watangazaji wote wa kike kwa sababu Uislamu haujatuamuru kufunika nyuso zetu,” aliongeza Niazi.

Kufuatia hilo wapo pia watangazaji wa kiume walioungana na wale wa kike na kufunika nyuso zao pia wakiwa wanasoma habari.

 

error: Content is protected !!