Museveni : Kuleni mtama na mihogo

HomeKimataifa

Museveni : Kuleni mtama na mihogo

Hotuba ya Rais wa Uganda Yoweri Museveni kuhusu kupanda kwa bei ya bidhaa haikutoa ahueni kwa mamilioni ya Waganda ambao wako kwenye ukingo wa kutumbukia katika umaskini kutokana na kupanda kwa bei ya bidhaa muhimu kusiko na kifani ambako kumeondoa akiba yao.

Matarajio ya watu wengi kabla ya hotuba hiyo ni kwamba Museveni angeelezea hatua ambazo serikali inachukua kuwakinga Waganda kutokana na kupanda kwa bei hasa za bidhaa kama vile mafuta, nyenzo muhimu katika uzalishaji na usafirishaji wa bidhaa.

Hasa, baadhi walikuwa na matumaini kwamba Uganda ingefuata njia ya Kenya ambapo Rais Uhuru Kenyatta alitia saini mswada wa nyongeza mwezi uliopita wa kutenga Kshs 34 bilioni (takriban Sh trilioni 1) kwa makampuni ya mafuta ili kuwaepusha wakazi dhidi ya kupanda kwa bei ya mafuta.

Badala yake, Museveni alisema kuwa kuchukua hatua kama hiyo (ruzuku) itakuwa ni kujiua na “itaharibu hifadhi zetu za kitaifa.”

“Ikiwa tutatoa ruzuku au hata kuondoa tu ushuru wa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje, kiwango cha matumizi ama kitaendelea kuwa kile kile, lakini wakati huu kila lita [ya petroli] ikichukua dola zaidi, au kwa kweli itaongezeka. Upotevu wa dola sasa utaongezeka kwa lita. ..,” rais alisema.

Alisema kutokana na mazingira ya sasa, Waganda hawana budi kuwa na fedha wakati wakisubiri bei zishuke.

Rais Museveni amesema Waganda wanapaswa kula vyakula vya bei nafuu lakini vyenye virutubishi vingi kama vile mtama na mihogo na kuacha bidhaa za bei ghali kama mkate uliotengenezwa na ngano, ambao aliutaja kuwa “usio na afya.”

Alisema dawa halisi ya kupunguza wimbi la bei ni Waganda kuzalisha zaidi, jambo ambalo wengine wanasema haliwezi kustahimilika katika mazingira ya sasa kutokana na kupanda kwa bei ya pembejeo muhimu.

Museveni, kama ambavyo amekuwa akisema mara nyingi, alilaumu bei ya juu ya bidhaa kwa sababu mbili za nje: Kutatizwa kwa minyororo ya usambazaji na Covid-19 na Vita vya Urusi-Ukraine.

 

error: Content is protected !!