Chanzo cha watu kupigwa mawe Arumeru

HomeKitaifa

Chanzo cha watu kupigwa mawe Arumeru

Mkoani Arusha, wilayani Arumeru, wananchi wamekuwa wakipigwa na mawe kwa takribani wiki mbili sasa bila kujua mawe hayo yanatoka wapi.

Baada ya kuzungumza na waandishi wa habari, baadhi ya wananchi wametaja chanzo cha kupigwa mawe hayo ni mizimu kwani mawe hayo huanza kurushwa mida ya jioni na pale ambapo watu wamekusanyika na kuzungumzia tukio hilo.

Aidha, baadhi ya wananchi wanaunganisha tukio hilo na mgeni aliyehamia hivi karibuni katika eneo hilo lililoathiriwa zaidi.

Awali wananchi hao wanasema mawe yalikuwa yakianguka kutoka juu na kudondoka kwenye mabati ama vichwa vyao, lakini imefikia mahali hivi sasa mawe hayo yanavunja hadi vioo vya madirisha ya nyumba.

Ili kujiami na madhara yatokanayo na kurushiwa mawe hayo, wananchi wamekuwa wakivaa ndoo kichwani na kofia ngumu wanapotoka nje ya nyumba zao.

baadhi ya waandishi na polisi waliofika eneo hilo nao wamekuwa wahanga wa kupigwa mawe.

Uchunguzi kujua chanzo cha tatizo hilo na namna ya kulitatua bado unendelea kwa ushirikiano baina ya polisi na wananchi wa eneo hilo.

error: Content is protected !!