Mwanamke wa kwanza Afrika kuchezesha Kombe la Dunia

HomeBurudani

Mwanamke wa kwanza Afrika kuchezesha Kombe la Dunia

Akiwa na binti mdogo mwenye mapenzi makubwa na michezo, mara baada ya kuambiwa kuwa yeye ni mdogo sana kucheza mpira wa kikapu, aliamua kuhamishia mapenzi hayo kwenye mchezo wa mpira wa miguu ambao haukujali kimo chake.

Alizaliwa Rusizi, rwandwa. Shirikisho la Soka Rwanda (RFF) lilimkataa kujiunga na kozi ya ukocha kutokana na umri wake mdogo, hadi hapo alipofankiwa kuchezesha mchezo wa kwanza akiwa mwaka wake wa mwisho katika Shule ya Sekondari ya St. Vincent de Paul Musanze, mechi iliyomfungulia milango lukuki ya kufika mbali.

Alipomaliza shule alijifunza mpira na kuanza kwa kuchezesha mechi mbalimbali katika eneo alilokuwa akiishi na baadaye kufanikiwa kupiga hatua moja moja hadi kufikia kuamua mechi za wanaume daraja la pili.

Mwaka 2004, akiwa na miaka 33 tu, alifanikiwa kupata nafasi ya kwanza kwenye mchezo wa wanawake kati ya Tanzania na zambia kwenye kombe la CAF

Januari 2022, Salima Mukansanga alikuwa kocha mwanamke wa kwanza kuchezesha kombe la AFCON.

Mukansanga ameteuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kuwa muamuzi wa kwanza mwanamke kutoka Afrika kuchezesha mashindano ya Kombe la Dunia yatayofanyika Qatar kati ya waamuzi wengine 36 na waamuzi wasaidizi 69.

“Kwa njia hii, tunasisitiza wazi kwamba tunazingatia zaidi ubora na sio jinsia. Ningetumaini kwamba katika siku zijazo, uteuzi wa waamuzi wa kike wenye uwezo kwa ajili ya mashindano muhimu ya wanaume utachukuliwa kuwa jambo la kawaida na si la kustaajabisha tena,” alisema Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi ya FIFA, Pierluigi Collina.

 

error: Content is protected !!