Samia kutoa bilioni 100 kila mwezi

HomeKitaifa

Samia kutoa bilioni 100 kila mwezi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema serikali itatoa ruzuku ya Sh bilioni 100 kila mwezi kwa ajili ya kukabiliana na ukali wa bei ya mafuta mpaka hapo hali itakaporejea kuwa ya kawaida. 

Aliyasema hayo akizungumza na wananchi wa Bwanga wilayani Chato mkoani Geita wakati akiwa njiani kwenda mkoani Kagera kwa ziara ya siku tatu.

“Tunachofanya serikali ni kutoa ruzuku ya shilingi bilioni 100 kufidia katika mafuta ili bei zishuke na mwezi huu bei zimeanza kushuka,” 

“Tutaendelea kutoa hiyo ruzuku mpaka duniani kukae sawa. Tutaendelea kukata shilingi bilioni 100 kila mwezi kwenye matumizi ya serikali ili tuweke ruzuku kwenye mafuta,” alisema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia alisema Urusi ilikuwa inasambaza gesi ya kutosha katika nchi za Ulaya, hivyo kutokana na vita inayoendelea kati yake na Ukraine iliyoanza Gebriari mwaka huu, nchi za Ulaya ziliamua kugeukia mafuta ambayo Tanzania pia ilikuwa inanunua na kusababisha bei ya mafuta duniani kupanda.

error: Content is protected !!