Meya asema hakuna atakaye ondolewa milimani Mwanza

HomeKitaifa

Meya asema hakuna atakaye ondolewa milimani Mwanza

Baada ya taarifa iliyosambaa jana kuhusu kuhamishwa kwa wakazi wa milimani jijini Mwanza, Meya wa jiji hilo Constantine Sima amesema taarifa hizo sio za kweli na hakuna mtu atakaye ondolewa.

“Hakuna mwananchi atakayehamishwa maeneo ya Milimani na hii taharuki imekuja mara baada ya kupata ugeni wa Mh. Balozi wa Tanzania nchini Brazil alikuja na wawekezaji ambao walijielekeza kuwekeza katika maeneo mbalimbali moja ya sekta watakayowekeza ni kwenye sekta ya viwanda na utalii”

“Wawekezaji hawa walikuja kwa ajili ya kuifahamu Mwanza na kuangalia sehemu ya kuwekeza na suala la Milimani halikujadiliwa kabisa na hii taharuki imekuja mara baada ya kuonekana kwa wawekezaji hawa. Hakuna sehemu yoyote ambayo tumekubaliana na ilikuwa ni hatua za mwanzo kabisa za kuangalia sehemu za uwekezaji” alisema Sima Costantine, Meya Jiji la Mwanza.

Taarifa iliyosambaa jana ilisema kwamba, wawekezaji kutoka Brazil walikuja kwa ajili ya kuwekeza katika maeneo ya milimani hivyo wananchi wa eneo hilo wataondolewa na kulipwa fidia.

 

error: Content is protected !!