Daktari amfumua mgonjwa kidonda baada ya kushindwa kulipia

HomeUncategorized

Daktari amfumua mgonjwa kidonda baada ya kushindwa kulipia

Katika hali ya kushangaza mtaalamu wa afya ambaye hajafahamika amedaiwa kufumua nyuzi kwenye kidonda cha mgonjwa kwa madai mgonjwa huyo alishindwa kulipia gharama za matibabu.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeeleza kupokea kwa masikitiko makubwa taarifa hiyo inayozunguka mitandaoni.


“Ikiwa hili limetokea nchini Tanzania, basi ni ukiukwaji mkubwa wa huduma za kitabibu,” imeeleza taarifa ya wizara.

Kufuatia tukio hilo, wizara imeomba yeyote mwenye taarifa za wapi tukio lilipotokea au kituo gani awasilishe mara moja kwa namba ya huduma kwa mteja 199 ya wizara ya afya au atume ujumbe mfupi kwenye namba ya Waziri wa Afya ya 0734124191.

error: Content is protected !!