Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) leo Jumanne Julai 5, 2022 limetangaza matokeo ya mitihani ya kidato cha sita na kusema ufaulu umeongezeka kwa asilimia 99.87.
Akitangaza matokeo hayo visiwani Zanzibar leo Kaimu Katibu wa Baraza Hilo, Athuman Amas amemteja Catherine Alphonce Mwakasege kutoka shule ya St.Mary’s Mazinde Juu kuwa kinara wa matokeo hayo katika masomo ya sayansi mchepuo wa PCB.
Nafasi ya pili imechukuliwa na Lucy E Magashi kutoka shule ya St. Mary’s Mazinde Juu Tanga kutoka PCB. Muhewa Charles Kamando kutoka Tabora Boys, PCB akishika nafasi ya tatu akifuatiwa na Minael Simon Mgonja kutoka St.Mary’s Mazinde Juu mkoani Tanga PCB, aliyeshika nafasi ya nne.
Nafasi ya tano imechukuliwa na Norah Eliaza Kidjout kutoka shule ya St.Mary’s Mazinde Juu (Tanga) PCB, akifuatiwa na Jennifer Martin Chuwa aliyeshika nafasi ya sita kutoka St Mary’s Mazinde Juu, PCB.
Pauline Ildephonce Mabamba kutoka St.Mary’s Mazinde Juu Tanga PCM akichukua nafasi ya saba, Rachel Joachim Moshy amechukua nafasi ya nane kutoka St.Mary’s Mazinde Juu Tanga, akichukua mchepuo wa PCM.
Nafasi ya tisa na kumi imechukuliwa na Kulwa Mbizo Elias kutoka Tabora Boys, PCB na Oscar Eliakim Marabe kutoka Tabora Boys mchepuo wa PCB aliyechukua nafasi ya kumi.