Kiswahili lugha ya biashara Afrika

HomeKitaifa

Kiswahili lugha ya biashara Afrika

Wakati nchi wanachama wa jumuiya hiyo wakikutana leo Zanzibar katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Kiswahili duniani, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Dk Peter Mathuki amesema wananchi wa bara la Afrika wajiandae kunufaika na lugha hiyo ikiwemo kibiashara.

Akizungumza katika mahojiano maalum na idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa Dk Mathuki amesema Dkt Mathuki amesema anafahamu kwamba lugha hii pia imekubalika na Muungano wa Afrika AU kutumika kama lugha rasmi.

“Tunafurahi lugha hii ni ya ulimwengu mzima na itatusaidia katika kufanya biashara hapa kwetu barani Afrika kwa kuwa AU wameitambua si tu kama lugha rasmi bali lugha ya kutumika katika biashara,” amesema.

Amesema lugha hiyo itasaidia hasa kwenye ukuaji wa jumuiya na kuelewana kwa mambo tofuati.

“Wananchi wanaweza kuwasiliana baina ya nchi na nchi, wataweza kufanya biashara na kukubaliana kwa kutumia lugha ya Kiswahili,” amesisitiza Dk Mathuki.

Tayari Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limeitambua na kuikubali lugha ya Kiswahili kwa umuhimu wake na kuitengea siku rasmi ya kuadhimishwa Julai 7 kila mwaka.

Amewakumbusha watu wote wanaozungumza Kiswahili kuendelea kukienzi na kuhamasisha wengine wazungumze lugha hiyo.

Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na viongozi wote wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo.

Siku ya Kiswahili duniani inaadhimishwa kwa mara ya kwanza mwaka huu visiwani Zanzibar lakini kwa miaka inayofuata  itakuwa inaadhimishwa katika nchi tofauti za EAC.

error: Content is protected !!