Shirika la Reli Tanzania (TRC) linafanya utafiti wa kuwa na reli katikati ya maji likiwamo la Mwanza, Arusha, Mbeya na Dodoma na kuziunganisha na viwanja vya ndege.
Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kdogosa amsema mwishoni mwa Agosti, mwaka huu treni ya mkandarasi inayotumia dizeli itaanza majaribio kutoka Dra es Salaam hadi Dodoma baada ya kukamilika kwa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro kwa asilimia 97.
“Kwenye kituo kikuu cha reli kutakuwa na kituo cha mabasi ya mwendo kasi ambacho kitatumika baada ya abiria wanaoshuka na kwenda maeneo mbalimbali ndani ya jiji husika. Tunaendelea na utafiti kuona namna ya kujenga reli itakayokwenda Uwanja wa Ndege, Kigamboni na Mwenge hadi Tegeta(Dar es Salaam),” alisema Kadogosa.