Hatua atakazo fanya Mfalme Charles III

HomeKimataifa

Hatua atakazo fanya Mfalme Charles III

Kufuatia kifo cha Malkia Elizabeth, Mkuu wa zamani wa Wales, Charles, amerithi kiti cha ufalme bila sherehe yoyote. Hata hivyo, kuna idadi ya hatua za utendaji na za kitamaduni ambazo lazima apitie ili kutawazwa kuwa Mfalme.

1. Kuhusu Jina
Toka jana, tumefahamu kuwa Charles sasa anakuwa Mfalme Charles III. Angeweza kuchagua jina lolote miongoni mwa majina yake – Charles, Philip, Arthur, George.

Pia jina la mke wa Charles, Camila, nalo limebadilika. Sasa atafahamika kama Malkia Consort – consort ikimaanisha mke wa mfalme.

2. Kuhusu sherehe rasmi
Inatarajiwa kuwa, Charles atatangazwa rasmi kuwa Mfalme siku ya Jumamosi mbele ya Baraza la Upataji katika Jumba la St. James huko London. Baraza hilo huundwa na wajumbe wa Baraza la Faragha – kikundi cha wabunge wakuu wa zamani na wa sasa pamoja na baadhi ya watumishi waandamizi wa serikali, makamishna wakuu wa Jumuiya ya Madola na Meya wa London.

Zaidi ya watu 700 wanaruhusiwa kuhudhuria, lakini kutokana na notisi fupi, huenda idadi halisi ikawa ndogo sana. Katika Baraza la mwisho la 1952, karibu watu 200 walihudhuria.

3. Tamko la Mfalme (uapisho)

Tofauti na ilivyo kwa nchi zinazo ongozwa na Rais kama Mkuu wa nchi, Mfalme wa Uingereza hata apishwa. Badala yake huwa kuna tamko linatolewa na kiongozi mpya, Mfalme/Malkia.

Kulingana na mila iliyoanza tangu karne ya 18, Mfame Charles III atafanya kiapo cha kulinda Kanisa la Scotland akihudhuria mkutano wa pili wa baraza la Upatanishi na Baraza la Faragha (Privy Council) ambapo atatamka “Mungu mlinde Mfalme”.

4. Kuvishwa Taji Rasmi

Mfalme Charles III atavishwa taji rasmi katika sherehe maalumu ya kutawazwa ambayo inaweza kufanyika baadaye sana. Mfano, Malkia Elizabeth alirithi kiti cha enzi Februari 1952 na alitawazwa Juni 1953.

Kwa miaka 900 iliyopita kutawazwa kumefanyika huko Westminster Abbey – William the Conqueror alikuwa mfalme wa kwanza kutawazwa huko, na Charles atakuwa wa 40.

5. Mkuu wa Jumuiya ya Madola
Charles amekuwa mkuu wa Jumuiya ya Madola, chama cha nchi huru 56 na watu bilioni 2.4. Kwa nchi 14 kati ya hizi, pamoja na Uingereza, Mfalme ndiye mkuu wa nchi.

error: Content is protected !!