Maambukizi ya Uviko-19 yapungua nchini

HomeKitaifa

Maambukizi ya Uviko-19 yapungua nchini

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema kasi ya maambukizi ya ugonjwa wa Uviko-19 nchini imepungua kutokana na hatua mbalimbali zinazochukuliwa kudhibiti ugonjwa huo.

Ummy katika taarifa ya mwenendo wa maambukizi ya Uviko-19 iliyotolewa leo Septemba 8,2022 imeeleza kuwa pamoja na kasi ya maambukizi mapya kupungua tayari asilimia 60 ya walengwa wa chanjo ya Uviko-19 wameshachanja.

Hata hivyo taarifa hiyo imeonya kwamba watu waendelee kuchukua tahadhari za ugonjwa huo ikiwemo kupata chanjo.

error: Content is protected !!