Mbaroni kwa kuuza jezi za feki za Simba na Yanga

HomeKitaifa

Mbaroni kwa kuuza jezi za feki za Simba na Yanga

Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linamshikiria Said Furaha (31) kwa tuhuma za kukutwa na jezi feki za timu za Simba na Yanga dazani 296.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ramadhan Ng’anzi aliyekuwa akizungumza na waandishi wa habari Julai 13, 2022 amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa Julai 5 mwaka huu katika eneo la Pamba road Sokoi Wilaya ya Nyamagana.

Amesema kuwa kati ya jezi hizo dazani 145 ni za nembo ya klabu ya Simba na dazani 151 ni za kablu ya Yanga inayofadhiliwa na kampuni ya GSM.

Kamanda Ng’anzi amesema walipata  taarifa toka kwa afisa masoko wa kampuni ya GSM na Vunja bei kuwepo kwa mfanyabiashara anayesambaza na kuuza jezi hizo bandia.

“Baada ya taarifa hizo ufuatiliaji wa kina na haraka ulifanyika na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa tajwa hapo juu akiwa na jezi hizo bandia za klabu ya Simba na Yanga dukani kwake,” amesema  Kamanda Ng’anzi.

Amesema polisi wanaendelea kufanya upelelezi wa kina kuhusiana na shauri hilo ili kuweza kubaini mtandao mzima wa wahusika wote wanaotengeneza, kuagiza na kuingiza nchini bidhaa hizo bandia suala linachongangia wadhamini wa klabu hizo kukosa mapato.

“Upelelezi wa shauri hili unakamilishwa mara moja na mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani haraka iwezekanavyo,” amesisitiza kamanda huyo.

error: Content is protected !!