Bandari ya Dar inavyoimarisha soko la biashara

HomeKitaifa

Bandari ya Dar inavyoimarisha soko la biashara

Ripoti mpya ya GBS Africa imeonyesha kwamba upanuzi mkubwa na uboreshaji wa ufanisi katika bandari kuu ya Tanzania ya Dar es Salaam umeiwezesha kutoa masuluhisho ya biashara na usafiri yenye gharama nafuu ikilinganishwa na bandari nyingine.

Kulingana na ripoti ya kampuni ya huduma za ushauri, Bandari ya Dar es Salaam inakuwa kitovu cha kikanda cha kubadilisha bidhaa na kuagiza kwa Tanzania na nchi zake zilizounganishwa na ardhi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).

“Nchi zisizo na bandari kama vile Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Malawi, Uganda, Zambia, Rwanda na Zimbabwe zinazidi kuchagua Dar es Salaam badala ya Mombasa kutokana na matatizo ya msongamano wa nchi hizo,” taarifa hiyo inasema.

Baadhi ya bidhaa zinazosafirishwa bandarini kuwa ni madini ya shaba pamoja na mazao ya kilimo kama vile chai, kahawa, tumbaku, mbegu za mafuta, pamba, mkonge na korosho.

Wakati miradi ya upanuzi na ununuzi wa vifaa vya kisasa katika Bandari ya Dar es Salaam ukiendelea, serikali imekuwa na shauku ya kuvutia wafanyabiashara na wawekezaji hali inayoongeza uagizaji wa bidhaa na mauzo ya nje kupitia bandari.

Tangu Rais Samia Suluhu Hassan ashike wadhifa wa juu wa nchi Machi, mwaka jana, kuvutia wafanyabiashara na uwekezaji imekuwa miongoni mwa vipaumbele vyake vikuu.

Kulingana na ripoti ya 2020 ya Bandari ya Afrika: Ripoti ya Mabadiliko ya Haraka, bandari zinazokua za Afrika ni Lagos, Dar es Salaam, Mombasa na Cape Town. Lakini ili Dar es Salaam iweze kufanya vizuri zaidi maboresho ya haraka yanaitajika kufanyika bandarini ikiwemo pamoja na kutoingezea mkataba TICTS iliyoshindwa kufanya kazi yake kwa ufanisi kwa miaka 20.

error: Content is protected !!