CCM yapongeza jitihada za Rais Samia kuiwezesha DIT

HomeKitaifa

CCM yapongeza jitihada za Rais Samia kuiwezesha DIT

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, amesema Chama Cha Mapinduzi kimeridhishwa na hatua zinazochukuliwa na Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kuiwezesha Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT) kutekeleza mradi wa ujenzi wa vituo vya umahiri ambapo zaidi ya Sh. bilioni 100 zimewekwa na Serikali.

Akizungumza leo baada ya kufanya ziara fupi DIT, Shaka amesema wamekuwa wakienda maeneo mbalimbali kukagua na kuangalia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/2025 katika mashirika na taasisi ambazo zimepewa dhamana na Serikali.

“Kumekuwa na jitihada kubwa zinazofanywa na Chama Cha Mapinduzi kupitia Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia kwenye uwekezaji wa fedha nyingi za maendeleo maeneo mbalimbali .Moja ya eneo ambalo pengine hatujafika kuona namna ambavyo fedha zimewekwa na utekelezaji unaendelea ni eneo hili lililobeba teknolojia.

“Nikisema teknolojia tunamanisha mfumo mzima wa mabadiliko haya ya kidunia na hapa nazungmzia TEHAMA, leo tumepata fursa hii kuona namna ambavyo wenzetu wa DIT wanatumia utaalamu huu kubadilisha miundombinu hii ya magari kutoka kwenye mafuta kwenda kwenye gesi.

Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi ya DIT Preksedis Ndomba alisema wanaishukuru Serikali kwa kufanya uwekezaji mkubwa kwenye taasisi hiyo na kazi iliyopo mbele yao ni kuhakikisha wanatekeleza miradi ya ujenzi wa vituo vya umahiri huku akitumia nafasi hiyo kuelezea kwenye ufungaji wa mifumo ya kutumia gesi kwenye magari wameendelea na sasa wameshafunga kwenye magari 1000 na miongoni mwao yamo magari ya Serikali.

error: Content is protected !!