Zijue njia 3 za asili za kukuza matiti

HomeElimu

Zijue njia 3 za asili za kukuza matiti

Hauhitaji kufanyiwa upasuaji wala kutumia madawa ili kuongeza matiti yako kwani unaweza kupata matokeo tofauti na jinsi ulivyo tegemea au madhara makubwa ya kiafya.Zifuatazo ni njia 3 za asili unazoweza kutumia kuongeza ukubwa wa matiti.

1. Kuongezeka kwa mwili
Matiti hutengenezwa kwa tishu zenye mafuta mengi, na ndizo zitakazoamua ukubwa wa matiti yako. Hivyo endapo utanenepa na kuongezeka mwili basi matiti nayo yataongezeka umbile lake na kuwa kubwa. Kula milo kama maziwa, papai, soya na karanga ili kuongeza ukubwa wa matiti.

2. Tumia mafuta ya massage
Kutumia mafuta ya ‘flaxseed’, ‘olive oil’, ‘jojoba oil’ na ‘fennel oil’ kukanda matiti yako kutasababisha kuongezeka. Mafuta haya huongeza mtiririko wa damu kwenye matiti, ukuaji wa mafuta kwenye matiti na kuchochea homoni zinazoongeza ukubwa wa matiti.

3. Kufanya mazoezi
Mazoezi yanaweza kuboresha saizi, nguvu, na mwonekano wa misuli ya kifuani iliyo chini ya matiti yako. Jaribu mazoezi kama vile kushinikiza dumbbell kifuani, ‘push-ups’, na ‘dumbbell pullovers’.

Hata hivyo usawa wa homoni unaosababishwa na ujauzito,kunyonyesha, wanawake waliotoka kujifungua na  na hedhi inaweza kusababisha ongezeko la ukubwa wa matiti.

error: Content is protected !!