Harmonize akasirishwa, atema nyongo

HomeBurudani

Harmonize akasirishwa, atema nyongo

Staa wa muziki kutoka nchini Tanzania, Harmonize ambaye pia ni balozi wa usafi jijini Dar es Salaam aliyeteuliwa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa huyu Mh. Amos Makalla ameonyesha kuchukizwa na watu wanaochafua fukwe za bahari kwakutupa chupa za plastiki, chupa na soda na uchafu mwingine katika maeneo ya fukwe za bahari.

Harmonzie amesema kwamba sio vizuri kutupa taka katika maeneo ambayo sio stahiki kwani ni uharibifu wa mazingira, pia aliongeza kuwa kila mtu anapaswa kuhakikisha mazingira yakuwa safi kwani kama bahari ni sehemu moja wapo ambayo watalii wengi hupenda kwenda hivyo kama itakuwa chafu basi itaharibu sifa.

Eric Omondi awaomba mashabiki kutohudhuria tamasha la Ali Kiba na Harmonize Kenya

“Mimi ni balozi wa usafi Dar es Salaam lakini haimaanishi kwamba sio balozi wa mikoa mingine bali ni wa Tanzania nzimaa, kama mtu unaenda beach nakutupa chupa na uchafu wewe huna akili kwani unaharibu utamaduni, kuna watu wengi wanatoka nje nakuja Tanzania kwani wanaamini watakuta fukwe safi hivyo basi usitupe taka katika sehemu ambazo sio stahiki,” alisema Harmonize.

Mmiliki huyo wa lebo ya Konde Gang alienda katika fukwe za bahari ya Imara Resort, Zanzibari akiwa na mchumba wake mpya mrembo Briana ambaye pia alionesha ushirikiano wakuokota uchafu na kuuweka katika sehemu inayostahili.

error: Content is protected !!