Mtanzania arudishwa kutoka India baada ya kugundulika na kirusi kipya cha UVIKO-19

HomeKitaifa

Mtanzania arudishwa kutoka India baada ya kugundulika na kirusi kipya cha UVIKO-19

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Profesa Abel Makubi amesema Serikali imeanza kufuatili taarifa za abiria aliyerudishwa na Serikali ya India akitokea Tanzania baada ya kudaiwa kuwa na virusi vipya vya wimbi la nne la UVIKO-19 vinavyo julikana kama Omicron.

Prof Makubi anasema kulingana na taarifa za za Maabara kuu ya Taifa hadi sasa hakuna mtu ambaye amebainika kuwa na virusi vipya vya wimbi la nne la UVIKO-19 kama inavyodaiwa, alieleza kuwa kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini India wanafuatalia ili kubaini ukweli wa jambo hilo na baadae kuchukua hatua stahiki. Taarifa rasmi bado hazijithibitisha kama mtu huyo alitoka Tanzania moja kwa moja au alipita Tanzania na kwenda India.

Maabara ya Taifa imekuwa ikichunguza mabadiliko ya Virusi (Gene Sequencing), kwa kuangalia uwepo wa anuwai mbalimbali zinatokana na mabadiliko ya Uviko-19 ikiwemo anuwai mpya ya Omicron. Prof Makubi akaongezea kwa kusema maabara hiyo ina uwezo wa kubaini anuwai mpya ya Omicron wanaendelea kuzifuatilia sampuli zote wakibaini uwepo wa anuwai mpya ya Omicron.

Pamoja na yote alisema wananchi wanatakiwa kutokuwa na hofu bali waendelee kuwa watulivu, kutekeleza shughuli za maendeleo huku wakiendelea kuchukua tahadhari mbalimbali dhidi ya ugonjwa huo kama kunawa mikono na sabuni na maji tiririka, kujiepusha na msongamano isiyokuwa ya lazima pamoja na kuvaa barakoa.

error: Content is protected !!