Serikali kutumia tiktok

HomeKitaifa

Serikali kutumia tiktok

Mbunge wa Viti Maalum, Martha Gwau ameishauri Wizara ya Maliasili na Utalii kutumia mitandao ya kijamii kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii huku akitoa mfano wa namna TikTok inavyoweza kusaidia kuleta Watalii.

“Nimefanya utafiti kwenye nchi za jirani za Afrika na nchi za wenzetu zilizoendelea. Nimeona juzi tu hapa Kenya imeingia mkataba na mtandao wa tiktok, tiktok ni mtandao wa vijana na watu wengine wanautumia kwa ajili ya ku-post vitu mbalimbali, wametengeneza video fupi ambazo zinaonyesha utalii wao,” alisema Mbunge Gwau.

Gwau ameishauri Wizara hiyo kujikitaka kwenye utangazaji wa utalii kwa njia ya kidigitali kwa kile alichodai kwamba siku hizi watu wengi wanapenda kufuatilia mambo kwenye mitandao.

Pia, alishauri kuongezeka kwa programu mbalimbali zitakazoweza kuchochea ukuaji wa soko la utalii kama ambavyo filamu ya Royal Tour iliyoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.

 

error: Content is protected !!