Eric Omondi awaomba mashabiki kutohudhuria tamasha la Ali Kiba na Harmonize Kenya

HomeBurudani

Eric Omondi awaomba mashabiki kutohudhuria tamasha la Ali Kiba na Harmonize Kenya

Zikiwa zimebaki siku chache kufanyika kwa tamasha la Afro Vasha nchini Kenya, huku wasanii kutoka Tanzania Alikiba na Harmonize wakiwa kwenye orodha ya wasanii watakotumbuiza siku ya tarehe 11 na 12, mchekeshaji Eric Omondi amewaomba mashabiki kutohudhuria kwakile anachodai kwamba wanamuziki wa Kenya wapewe haki.

https://clickhabari.com/jela-miaka-mitano-kwa-kuuza-albamu-ya-alikiba-mtaani/

“Ninatoa wito kwa kila Mkenya kususia tukio hili. Hawa waandaaji hawana heshima sana. Tulikubali kuwa hatuhudhurii tukio lolote ambalo linadharau kwa nini wasanii wetu wanaonyeshwa katika mabango kwa kuwekewa picha ndogo. Ninawapa waandaaji saa 3 kurekebisha tangazo hili la kipumbavu na wasipofanya hivyo nitahakikisha hakuna mtu anayehudhuria tamasha hili. Niamini  wewe Afrovasha nakushauri. Badilisha hilo tangazo,” ameandika Omondi.

Taarifa hiyo aliyoiandika kwenye ukurasa wake wa Instagram umepokelewa tofauti na alivyotegemea kwani maoni ya wengi wanapinga kile alichosema huku wakimtaka aachane na mpango wake huo wakutaka kufanya watu wasihudhurie tamasha hilo.

error: Content is protected !!