Nandy, Zuchu wadharauliwa Nigeria

HomeBurudani

Nandy, Zuchu wadharauliwa Nigeria

Wasanii wa kike wanaofanya vizuri kwenye muziki wa Bongo Fleva Zuhura Othman maarufu kama “Zuchu” na Faustina Charles Mfinanga maarufu kama “Nandy”, walihudhuria hafla ya utoaji tuzo za muziki za AFRIMMA zilizofanyika nchini Nigeria Novemba 22 mwaka huu. Wasanii hao wanasema walipitia mengi ambayo hayakustaili ikiwemo kudharauliwa nchini humo.

Zuchu na Nandy walichaguliwa kuwania miongoni mwa tuzo zilizokua zinatolewa, lakini pia Zuchu alikua anatumbuiza katika tamasha hilo. Katika moja ya mahjiano aliofanya Nandy karibuni alisema kuwa hata kama kama hawakushinda tuzo walistahili kutendewa vizuri.

“Tunalalamika haukuwa wakati sahihi wa kusema wakati ule tunarudi, mtasema kwa sababu tumekosa tuzo sio kwamba hatustahili tuzo, Zuchu anastahili tuzo, mimi nastahili tuzo, kila mtu anastahili pia. Hatupingi kwa ile tuzo waliyompatia binti wa Kenya.”

Kumbe Zuchu anachukua 25%

“Lakini kuna ile treatment mtu kuona angalau sijapata tuzo, sijapoteza muda kuna hiki, treatment ambayo nimepata kwa hawa watu ni nzuri ambayo next time nitafikiria kwenda tena, lakini treatment haikuwa nzuri kila mmoja analalamika kivyake” amesema Nandy.

Pamoja na kufunguka yote hayo Nandy anasema Zuchu alipofika alikosa hata pa kulala ikabidi akatafute sehemu ya nyingine. Nandy alimalizia kwa kusema inabidi sasa wasanii kutoka Bongo wajitafakari ni nini watafanya ili kuacha kushobokea Wanaigeria.

“Mara kina Zuchu wamefika hamna sehemu ya kulala, wameenda kulala sehemu nyingine, yaani na vitu vingine vingine siwezi kuvizungumzia. Zuchu alikuwa kwenye mazoezi, akaja msanii mkubwa wa Nigeria, akaambiwa muda umeisha, lakini Menejimenti yake ipo wazi ikawaambia huyu atamaliza ndio aingie huyo. Ukitoka hapo unajihisi huyo kanionaje? yaani mimi sistahili kufanya mazoezi yangu nikamaliza yakawa mazuri?” ameongeza Nandy.

error: Content is protected !!