Maombi ya kesi ya Makonda yaondolewa na kurudishwa Mahakamani

HomeKitaifa

Maombi ya kesi ya Makonda yaondolewa na kurudishwa Mahakamani

Maombi ya kufungua kesi dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, yaliyowekwa na mwandishi wa habari Saed Kubenea, yamesikilizwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondo.

Awali, mawakili wa Saed Kubenea waliomba kuondoa maombi yao Mahakamani hapo, baada  ya kugundulika kwa kasoro mbalimbali katika maombi yao, hususan kasoro za kiuandishi.

Baadhi ya kasoro zilizojitokeza ni kukosewa kwa jina la mshtakiwa wa tatu (Paul Makonda) katika maombi hayo pamoja na majina ya mwasilisha maombi na ya aliyeapa kuwa tofauti na baadaye kukubaliana na maombi ya mawakili wa upande wa Kubenea.

https://clickhabari.com/huu-ndio-utajiri-wa-paul-makonda/

Baadae, mawakili wa Kubenea walirudisha upya maombi yao ya kumshtaki Paul Makonda pamoja na Ofisi ya mwendesha mashtaka na Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai kwa madai ya kushindwa kuchukua hatua dhidi ya Paul Makonda wakati akiwa Mkuu wa Dar es Salaam (Kuhusu madai ya kuvamia ‘Clouds Media’ na matumizi mabaya ya madaraka).

Kinachosubiriwa sasa ni Mahakama kupanga tarehe ya kusikiliza shauri hilo.

error: Content is protected !!