Wanaohifadhi wahamiaji haramu waonywa, ‘Sakasaka’ yaanza

HomeKitaifa

Wanaohifadhi wahamiaji haramu waonywa, ‘Sakasaka’ yaanza

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala amewaonya Watanzania wanaowatumia wahamiaji haramu kama chanzo cha kipato kuacha mara moja tabia hiyo kwani huchochea ongezeko la wahamiaji haramu.

Akizungumza mara baada ya kuwasili Morogoro Machi 22, 2022 kwaajili ya kukagua karakana la wahamiaji haramu, Dkt. Makakala amewataka pia wananchi kuwa wazalendo huku akisifu mkoa wa Morogoro kwa jitihada wanazozifanya kukabili uhamiaji haramu.

“Morogoro inafanya vizuri kwa kuongoza kukamata wahamiaji haramu wanaoingia nchini, ndiyo maana hata katika kuongeza nguvu tutaiangalia Morogoro kipekee,” alieleza.

Dkt. Makakala pia ametangaza wiki moja ya msako wa wahamiaji haramu iliyopewa jina la ‘Sakasaka’ inayolenga kukagua uhalali wa wageni waliopo nchini ili kujiridhisha kama wamekidhi vigezo na masharti.

“Katika kudhibiti wahamiaji haramu kutoka Ethiopia ambao wamekuwa wakikwama kuendelea na safari zao na wengine kuishia katika vifungo magerezani, tumekuja na mfumo wa viza rejea ambao utatoa uelekeo wa namna ya kupambana na usumbufu unaojitokeza wa matumizi ya nija za panya,” alisema Dkt. Makakala.

Vijana 820 wamefanikiwa kupata ajira uhamiaji na watasambazwa katika mikoa yote ili kupambana na adha ya uhamiaji haramu.

error: Content is protected !!