Wazazi wachochea binti kujinyonga kisa mapenzi

HomeKitaifa

Wazazi wachochea binti kujinyonga kisa mapenzi

Binti mmoja mkaaji wa Kaskazini Unguja, Zanzibar amefariki baada ya kujinyonga kwa kamba ya katani chumbani kwake mchana wa Machi 16.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kaskazini Unguja, Martin Leo Otieno amesema Saida Buruhan Haji (20), mkaaji wa Bumbwini Makoba alichukua uhai wake kwa kujinyonga kwa kamba aliyoitundika katika dirisha la chumba chake, baada ya wazazi wake kumtaka avunje mahusiano yake na mpenzi wake.

Wazazi na ndugu wa binti huyo walimgombeza na kumtaka amuache mpenzi wake na kuacha mahusiano ya kimapenzi mpaka atakapoolewa, jambo ambali binti huyo hakulipokea vizuri.

Kamanda Otieno amewasihi wazazi na ndugu kutafuta amna nzuri ya kuzungumza na vijana wao hasa mabinti kuhusiana na masuala ya mahusiano na wakati gani waanze mahusiano.

 

error: Content is protected !!