Kikwete ampa tano Rais Samia Suluhu

HomeKitaifa

Kikwete ampa tano Rais Samia Suluhu

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk Jakaya Kikwete, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wa kuunda kikosi kazi cha ukusanyaji wa maoni, kuhusu masuala ya siasa na kusema uwepo wake utasaidia kupunguza joto la kisiasa lililopo nchini.

Akizungumza muda mfupi baada ya kuwasilisha maoni yake, Kikwete amesema kuundwa kikosi kazi hicho ni kitendo cha kiungwana na busara zilizofanywa na Rais Samia, kuhakikisha demokrasia inazidi kukua nchini.

“Nimefurahi nimepata nafasi ya kuja mbele ya kikosi kazi hiki, itasaidia kupunguza joto ndani ya nchi, matumaini yake kitatusaidia kutengeneza maridhiano na mwenendo mzuri wa kufanya shughuli za kisiasa hapa nchini,” amesema Kikwete.

Kuhusu maoni aliyoyatoa mbele ya kikosi kazi hicho, Rais Kikwete amesema amejibu kutokana na namna ambavyo aliulizwa maswali, hivyo wao ndiyo wana jukumu la kuelezea kile alichowasilisha.

error: Content is protected !!