Ziara ya Rais Samia Qatar inavyoleta matunda mema nchini

HomeKitaifa

Ziara ya Rais Samia Qatar inavyoleta matunda mema nchini

Inafahamika kwamba huwezi kufanikiwa na kusonga mbele ukiwa peke yako, lazima ushirikiane na watu ili uweze kupata ujuzi zaidi na maarifa yatakayokusaidia kufika pale unataka.

Rais Samia Suluhu Hassan ameshuhudia utiaji saini wa makubaliano ya ushirikiano kati ya Chemba ya Biashara ya Tanzania, Zanzibar na Chemba ya Biashara ya Qatar.

Dhumuni la mkataba huo ni kuimarisha Biashara na Uwekezaji kati ya wafanyabiashara wa Tanzania na Qatar hususan kwenye sekta za utalii, miundombinu, ujenzi wa mahoteli na usambazaji wa gesi.

Katika kuhakikisha mazingira ya ufanyaji biashara yanakuwa rafiki, Rais Samia amezungumza na Waziri wa Fedha wa Qatar, Mhe. Ali bin Ahmed Al-Kuwari ambapo wamejadili masuala ya kikodi baina ya nchi hizo mbili.

Pande zote mbili zimekubaliana kubadilishana uzoefu kwenye sekta ya afya hasa katika huduma za kibingwa na za dharura ikiwa ni moja wapo ya njia inayoenda kuleta mageuzi makubwa kwenye sekta ya afya nchini Tanzania.

 

 

error: Content is protected !!