Bei elekezi za gesi asilia kwa ajili ya magari

HomeKitaifa

Bei elekezi za gesi asilia kwa ajili ya magari

Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) inakamilisha mchakato wa kuanza kutoa bei elekezi za gesi asilia kwa ajili ya matumizi ya magari.

Pia, imeeleza kuwa haijaanza mchakato wa kutoa bei elekezi kwa ajili ya gesi ya kupikia nyumbani (LPG), hadi tatizo la miundombinu ya kushushia gesi hiyo litakapotatiwa ufumbuzi ili meli kubwa zinazobeba bidhaa hiyo ziweze kushusha gesi hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Modestus Lumato alisema hayo jana wakati akizungumiza kuhusu mfumo huo wa utoaji bei elekezi kwa bidhaa za gesi.

“Tunatengeneza bei za gesi asilia inayotoka Songo Songo (CNG). Mchakato tunao uko kwenye hatua ya mwisho muda si mrefu labda hadi Januari, mwakani tutakuja na bei elekezi ya gesi hii,” alieleza Lumato.

Alisema Mchakato huo ukikamilika utawasilishwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kisha kutolewa kwenye Gazeti la Serikali ndipo bei hizo elekezi zitaanza kutolewa.

Alieleza sababu za mamlaka hiyo kuanza kutoa bei hiyo elekezi kuwa ni matakwa ya wawekezaji wanaokusudia kuanzisha vituo vya gesi ambao wanataka kufahamu bei watakayouzia gesi hiyo ili kujua watapata faida kiasi gani.

 

error: Content is protected !!