Kicheko bei mpya za petroli na dizeli

HomeKitaifa

Kicheko bei mpya za petroli na dizeli

Dar es Salaam. Huenda itakuwa kicheko na maumivu kwa watumiaji wa nishati ya mafuta baada ya kutolewa kwa bei mpya zinazoonyesha kupanda na kushuka kwa petroli na dizeli kwa Disemba 2022. 

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa hapa nchini ambazo zimeanza kutumika leo Desemba 7 ,2022.

Bei ya mafuta ya rejareja ya petroli yanayoingia kupitia bandari za Dar es Salaam na Mtwara imepungua kwa Sh59 kwa lita na Sh92 kwa lita, mtawalia, ikilinganishwa na bei za Novemba 2022.

Hiyo ina maana kuwa petroli kwa upande wa Dar es Salaam imeshuka hadi kufikia Sh2,827 kutoka Sh2,886 iliyokuwapo Novemba.

Kwa bei hiyo ya Disemba, mmiliki mwenye gari, akiwa na Sh10,000 atapata lita 3.5 za petroli ikilinganishwa na lita 3.4 alizokuwa akipata Novemba.

Wenzao wa Mtwara wao watanunua petroli kwa Sh2,825 kwa lita kutoka Sh2,917 huku bei ya Tanga ikiongezeka kwa Sh9 kwa lita ikilinganishwa na bei ya mwezi uliopita.

Kulingana na ukomo wa bei ya mafuta iliyokuwapo Novemba mwaka huu, bei ya petroli kwa upande wa Tanga imefikia Sh2,815 kutoka Sh2,806.

“Hata hivyo, ili kuendelea kupunguza athari za ongezeko la bei za mafuta nchini ambapo shughuli nyingi za kiuchumi zinategemea dizeli, Serikali imetoa ruzuku kwa bei za Desemba 2022,” imeeleza Ewura, licha ya kuwa mafuta ya petroli kwa bandari ya Dar es Salaam hayana ruzuku.

“Kutokana na ruzuku hiyo, bei ya mafuta ya dizeli imepungua kwa Sh83 kwa lita, Sh247 na Sh243 kwa Dar es Salaam, Tanga na Mtwara.

Kutokana na ruzuku hiyo, dizeli inauzwa kwa Sh3,247 kutoka Sh3,052 ya Novemba mwaka huu kwa upande wa Dar es Salaam huku wakazi wa Tanga wakinunua Dizeli kwa Sh3,496 kutoka Sh3,249 na Mtwara kwa Sh3,512 kutoka Sh3,269

“Bei ya mafuta ya taa kwa bandari ya Dar es salaam imeongezeka kwa Sh141 kwa lita ukilinganisha na bei zilizopita kwa sababu ya wastani wa bei kubwa zaidi ya mafuta yaliyosafishwa katika soko la dunia na gharama za usafirishaji,” imeeleza Ewura.

error: Content is protected !!