Wengi wetu tumezoea asali kwa matumizi ya kula lakini kama ulikua hujui pia ni tiba ya ngozi pamoja na kuzui chunusi.
Kutokana na uwezo wa asali kuua bakteria na kuvuta uchafu katika matundu ya ngozi, asali itakusaidia kutatua tatizo la chunusi.
Kwa njia hii chukua asali mbichi kijiko kimoja cha chakula, changanya na mafuta ya nazi vijiko viwili.
Kisha changanya mchanganyiko wako uwe laini na paka usoni huku ukisugua taratibu kwa kufanya kama viduara, huku ukiepuka kufikisha machoni.
Asali pia inaweza kutumika kama kisafisha ngozi, hapa changanya kijiko kimoja asali na kijiko kimoja baking soda.
Tumia mchanganyiko huu kusugua ngozi yako.
Asali inaongeza lishe na chembe chembe za kuzuia madhara yanayotokana na sumu zinazozeesha ngozi wakati baking soda inasaidia kusafisha matundu ya ngozi.
Asali pia hutumika kulainisha ngozi kwa kuwa ina asili ya kuvuta unyevu kutoka kwenye hewa na kuipa ngozi uwezo wa kuhifadhi unyevu, hivyo ni faida kwa mtu mwenye ngozi kavu.