Nchini Tanzania, karibu theluthi moja (asilimia 31.8) ya kaya zinachukua mkopo kwa ajili ya mahitaji ya kujikimu ikiwemo chakula na malazi.
Kwa mujibu wa ripoti ya Kufuatilia Hali ya Kaya Tanzania (NPS) ya mwaka 2020/21 iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), asilimia 26.4 walichukua mkopo kwa ajili ya kununua pembejeo za biashara.
“Mwenendo huu ni kweli kwa jinsia ya mkuu wa kaya, na matumizi sawa ya mkopo/mikopo iliyopokelewa na wote wawili kaya zinazoongozwa na wanawake na wanaume,” imeeleza ripoti hiyo.
Ni watu wachache sana nchini Tanzania (asilimia 0.5) wanatumia mkopo kwa ajili ya kununua mashine za kilimo.