Baraza la Mitihani (NECTA) limefuta matokeo yote ya Watahiniwa wanne wa kidato cha nne mwaka 2022 walioandika lugha za matusi katika mitihani yao.
Baraza la Mitihani pia limeyafuta matokeo yote ya Watahiniwa 333, mmoja wa QT na 332 wa Mtihani wa kidato cha nne ambao wamebainika kuwa wamefanya udanganyifu kwenye mtihani.
“Matokeo hayo yamefutwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 (2) (I na J) cha Sheria ya Baraza la Mitihani
sura ya 107 kikisomwa pamoja na kifungu cha 30 (2) (b) cha kanuni za mtihani mwaka 2016”