Vijana wamvamia bibi, wamng’oa ndonya

HomeKitaifa

Vijana wamvamia bibi, wamng’oa ndonya

Vijana wanne katika kijiji cha Namangale walikamwatwa kwa kosa la kumvamia bibi kizee mwenye umri wa miaka 83 na kumng’oa ndonya yake mdomoni kwa lengo la kwenda kuiuza kwa tajiri mmoja anayeishi jijini Dar es Salaam.

Vijana waliohusika katika tukio hilo ni Saidi Mkonyange, Saidi Duda, Salum Nyagajage na Sudi Libui wote ni wakazi wa kijiji cha Nandandara, Kata ya Matambarale Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.

Baada ya kupata tenda hiyo vijana hao walikwenda na kumvamia bibi kizee huyo ambaye jina lake limehifadhiwa na kumjeruhi mdomoni wakati wa harakati wa kumnyofoa ndonya yake.

Aidha, vijana hao wameachiwa baada ya Bibi Kizee huyo kuwasamehe hasa baada ya kurudisha ndonya yake. 

 

error: Content is protected !!