CNOOC ya China kufanya utafiti wa mafuta na gesi baharini Tanzania

HomeKimataifa

CNOOC ya China kufanya utafiti wa mafuta na gesi baharini Tanzania

Kampuni ya CNOOC Ltd ya China inapanga utafiti wa mafuta na gesi baharani kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Petroli la Tanzania ( TPDC) wakati ambao nchi nyingi za Afrika Mashariki zikijitahidi kuendeleza rasilimali zake za asilia.

Taarifa kutoka kwa Waziri wa Nishati, January Makamba ni kwamba, kazi hiyo itafanywa katika maeneo ya bahari yenye uerefu wa 4/1B na 4/1C yanayoshikiliwa na TPDC.

Maeneo hayo yapo karibu na maeneo makubwa ya gesi yaliyogunduliwa na kikundi cha makampuni ya kimataifa ya nishati kinachoongozwa na Equinor ASA, Shell Plc, na Exxon Mbil Corp, ambayo yanapanga kujenga kituo cha gesi asilia iliyoyeyushwa chenye thamani ya dola za Kimarekani bilioni 42.

Ushirikiano wa TPDC na CNOOC ya China utakuza sekta ya mafuta na gesi nchini na kupelekea kuendelezwa kwa rasilimali za taifa na kuleta maendeleo endelevu kwa wananchi.

error: Content is protected !!