Rais Samia asisitiza usimamizi wa rasilimali kwa maendeleo ya wananchi

HomeKitaifa

Rais Samia asisitiza usimamizi wa rasilimali kwa maendeleo ya wananchi

Rais Samia Suluhu Hassan amewasihi viongozi wa Afrika kusimama imara na kutumia rasilimali zilizopo kwa maendeleo ya wananchi wao.

Ameyasema hayo alipokua akihutubia kwenye Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika nchini Kenya na kuhudhuriwa na wakuu mbalimbali wa nchi za Afrika na kusisitiza kwamba mchakato ubadilishaji wa malighafi kama madini kuwa bidhaa unafanyika ndani ya bara letu.

“Kwa kuzingatia wingi wa madini haya, bara hili linahitaji kubadilisha nafasi yake siyo tu kama msambazaji wa malighafi kwa dunia bali kwa kuimarisha minyororo ya thamani kuhakikisha kuwa ubadilishaji wa malighafi hizi kuwa bidhaa za kati na mwisho unafanyika ndani ya bara letu.

“Kama madini muhimu, yanapaswa kutoa mchango muhimu katika ukusanyaji wa mapato yetu ya ndani na kuundwa kwa ajira. Pia yanapaswa kuchangia kwa kiasi kikubwa katika ulinzi wa mazingira katika nchi zetu.” amesema Rais Samia

Akimaliza kuhutubia, Rais Samia aliwakaribisha viongozi hao kuja kushiriki Mkutano wa Kilimo na Chakula wa AGRF unaofanyika jijini Dar es Salaam.

“Kama mnavyofahamu, Tanzania inaandaa Mkutano wa Kilimo na Chakula wa AGRF wiki hii; Mkutano wa Viongozi utafanyika tarehe 7 Septemba, siku mbili zijazo. Kwa hiyo, napenda kutumia fursa hii kuwaalika tena Tanzania, na nitakuwa mwenyewe kule kuwakaribisha nyote.” amesema Rais Samia.

 

 

 

 

 

 

error: Content is protected !!