Kenya Commercial Bank (KCB) imeripotiwa kupungua kwa shughuli zake nchini Kenya na ukuaji imara ukishuhudiwa katika matawi yake ya nchi nyingine ndani ya miezi tisa ya mwanzo wa mwaka huu.
Wakati KCB Kenya ikionyesha kupungua kwa faida ya mtaji kwa 9%, matawi yake yalipo nchini Tanzania umeongezeka kwa 157% , Uganda kwa 129% na Sudan Kusini kwa 79%.
Aidha, mtaji wa Benki ya Equity Kenya umeshuka kwa 20% wakati ile ya DRC ukiongezeka kwa 142%, Tanzania umeongezeka kwa 136%, Rwanda kwa 46% na Uganda kwa 23%.
Kwa muonekano huo ni wazi kwamba kupungua huko kunatokana na mazingira magumu ya kiuchumi katika soko lake la ndani.