Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa maagizo kwa viongozi wa michezo nchini kuhakikisha wanaiendesha vyema sekta hii ili iweze kukuza vipaji vya vijana.
Ametoa maagizo hayo kwenye hafla ya chakula cha mchana alichowaandalia wachezaji na viongozi wa Timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 15 ( Karume Boys), Ikulu Tunguu , Zanzibar.
“Michezo ni biashara kubwa viongozi wa michezo badilikeni ili michezo iendeshwe kwa weledi, tuache kutegemea kuguna pasipopandwa na kuweka mipango endelevu yakuwekeza kwenye michezo ya vijana.” amesema Rais Samia
Ameyataka pia mabaraza ya michezo kuendelea kuratitu na kufuatilia utendaji wa vyama vya michezo na kuhakikisha vinaendeshwa na kujiendesha kwa manufaa ya taifa.
Agizo la mwisho alilolitoa Rais Samia ni kuhakikisha miundombinu ya michezo inayojengwa na kukarabatiwa itunzwe kwani inatumia gharama kubwa uharibifu unapotokea.
“Ujenzi wa miundombinu ya viwanja vya michezi ni gharama kubwa viwanja vote vinavyojengwa na kukarabatiwa vitumike kwa uangalifu na vifanyiwe matengenezo pale uharibifu unapojitokeza badala ya kusubiri uharibifu mkubwa maana jambo hilo linaongeza gharama.” amesema Rais Samia.