Rais Samia anavyowainua wamachinga

HomeKitaifa

Rais Samia anavyowainua wamachinga

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, amewaahidi wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama Machinga kuwashika mkono na kuwapa nguvu katika shughuli zao kwa kuwa ni kundi ambalo limeisaidia nchi kutengeneza nafasi za ajira.

Amesema hayo wakati wa kihutubia wananchi kwenye Mkutano wa Hadhara katika uwanja wa Samora mkoani Iringa, leo tarehe 12 Agosti, 2022, Rais Samia amesema

“Hawa watoto wangu wanalisaidia taifa katika kutengeneza ajira wameamua kujiajiri wenyewe na kwa sababu wameamua kujiajiri wenyewe serikali na mama atafanya kila analoweza kuwapa nguvu ili muendelee kujiariji.” amesema Rais Samia.

Pia, amewahakikishia kwamba serikali inaenda kujenda soko ili waweze kuwa na pahali pazuri pa kufanyia biashara zao.

“Ahadi yangu kwenu wanangu kama alivyosema Waziri wa fedha, soko lile tutalijenga tulimalize ilimpate pahali pazuri pa kufanyia biashara zenu,” amesema Rais Samia.

 

error: Content is protected !!