Viongozi watano walioambatana nao Rais Samia Vatican

HomeKitaifa

Viongozi watano walioambatana nao Rais Samia Vatican

Rais Samia Suluhu Hassan ameambata na viongozi watano wa vyama vya kitume vya Kanisa Katoliki Tanzania kwenda kumwona Kiongozi wa Kanisa hilo duniani, Papa Francis, huko Vatican, Roma.

Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Rais Samia atakutana na Papa Francis kwenye ofisi za Papa na kufanya mazungumzo ya faragha.

Wizara hiyo imeeleza kuwa baada ya mazungumzo hayo, Papa atakutana na ujumbe mzima wa Rais Samia ambao unajumuisha Mwenyekiti wa Halmashauri ya Walei Wakatoliki Tanzania, Prof. Deogratias Rutarora na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Walei-Zanzibar, Dalmas Gregory.

Viongozi alioambatana nao.

1. Bi. Eveline Ntenga – Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Wakatoliki Tanzania (WAWATA), Rais wa Wanawake Wakatoliki
Afrika.

2. Prof. Deogratias Rutatora – Mwenyekiti wa Halmashauri ya Walei Taifa.

3. Bwana Leonard Mapolu – Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA).

4. Bwana Dalmas Gregory – Mwenyekiti wa Halmashauri ya Walei Zanzibar.

5. Bi Teresia Seda – Mwenyekiti wa Utoto Mtakatifu Jimbo Kuu Dar es Salaam

Ziara hii inafuatia mwaliko wa Baba Mtakatifu Francis kwa Rais Samia.

error: Content is protected !!