Uboreshaji wa miundombinu ya bandari wakuza mapato

HomeKitaifa

Uboreshaji wa miundombinu ya bandari wakuza mapato

Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Mrisho Mrisho amesema maboresho yalifanywa na Serikali katika bandari za Tanzania yamechangia kwa kiasi kubwa ongezeko la mapato yanayokusanywa.

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa 13 wa Kitaaluma wa Jukwaa la Wahariri Tanzania ( TEF) kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Plasduce Mbossa, Bw. Mrisho alisema kiwango cha mapato kwa mwaka 2021 yalikuwa bilioni 800 huku mwaka wa fedha uliopita yalifika trilioni 1.3.

Mrisho amesema jambo lililochangia ongezeko hilo ni uboreshaji wa miundombinu iliyopo kwenye bandari zinazosimamiwa na TPA.

Mfano wa maboresho yaliyofanyika ni ujenzi wa gati la mita za mraba 300, sambamba na kutengwa mita za mraba 72,000 kwa ajili ya kuhifadhia shehena ya magari katika Bandari ya Dar es Salaam.

Ujenzi wa magati hayo sasa unawezesha meli kubwa kutia nanga katika Bandari ya Dar es Salaam.

error: Content is protected !!