Rais Samia: Wakati kuwekeza Tanzania ni sasa

HomeKitaifa

Rais Samia: Wakati kuwekeza Tanzania ni sasa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania ipo tayari kwa uwekezaji na hivyo wawekezaji na wafanyabiashara wachangamkie fursa hii.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kiwanda cha Kuunganisha Magari cha Saturn kilichopo Kigamboni, Rais Samia amesema Tanzania ipo tayari kwa uwekezaji na serikali itashirikiana na makampuni yatakayokuja kuwekeza.

“Niendelee kusisitiza Tanzania ipo tayari kwa uwekezaji, tuko tayari kupokea uwekezaji, acha makampuni yake tutashirikiana nayo tuone wapi wanakwenda kuwekeza.”

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa kuzindua Kiwanda cha Kuunganisha Malori na Matipa cha Saturn Corporation Limited kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Mei, 2024.

“Wakati wa kuwekeza ni sasa. Mazingira yapo mazuri, serikali ina ari ya kuhamasisha uwekezaji wa viwanda na mambo mengine kwahiyo wakati wa kuwekeza ni sasa na niwaombe sana msichelewe katika hilo.” amesema Rais Samia.

Taswira ya magari mbalimbali yaliyounganishwa katika Kiwanda cha Saturn Corporation Limited kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam

Aidha, katika uzinduzi huo Rais Samia amesema uwepo wa kiwanda hicho utachochea pia ukuaji wa sekta nyingine kama vile, kilimo, madini na usafirishaji.

error: Content is protected !!