Rais Samia: Shirika kama halifanyi vizuri liondoke

HomeKitaifa

Rais Samia: Shirika kama halifanyi vizuri liondoke

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa mashirika ya umma yasiyofanya kazi kwa tija hayana budi kufutwa. Akizungumza kwenye ufunguzi wa Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma, Rais Samia alieleza kuwa ni muhimu kwa mashirika hayo kuleta matokeo chanya kwa taifa, vinginevyo hayapaswi kuendelea kuwepo.

“Shirika tuliloliunda wenyewe kama halifanyi vizuri basi liondoke tu. Hatuwezi kwenda kulinda nafasi za watu na mashirika hayazalishi, hayana tija haiwezekani, madhumuni yetu mashirika yetu yafanye kazi, na ni madhumuni ya dunia nzima,” alisema Rais Samia.

Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan afungua Kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma Jijini Arusha

Alisisitiza kuwa lengo kuu la kuanzisha mashirika ya umma ni kuhakikisha yanatoa mchango mkubwa kwenye maendeleo ya taifa, na aliongeza kuwa ni maoni ya dunia nzima kuwa mashirika hayo lazima yawe na ufanisi ili yafae kuwepo.

Rais Samia ametoa wito kwa bodi na watendaji wakuu wa mashirika ya umma kuhakikisha kuwa wanaboresha utendaji kazi wa taasisi zao ili kufikia malengo yaliyowekwa.

error: Content is protected !!