Rais Samia: Nileteeni taarifa kuhusu Kibao

HomeKimataifa

Rais Samia: Nileteeni taarifa kuhusu Kibao

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amegiza Vyombo vya Uchunguzi kumpatia taarifa ya kina haraka kuhusu tukio baya la mauaji ya Kiongozi wa CHADEMA Ali Kibao na mengine ya namna hiyo.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X maarufu kama Twitter, Rais Samia amesisitiza kwamba serikali yake ya awamu ya sita haiungi mkono vitendo vya utekaji.

“Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa ya mauaji ya kiongozi wa CHADEMA Bwana Mohamed Ali Kibao. Natoa pole kwa viongozi wa chama hicho, familia ya Mzee Kibao, ndugu, jamaa na marafiki.

Nimeagiza vyombo vya uchunguzi kuniletea taarifa ya kina kuhusu tukio hili baya kabisa na mengine ya namna hii haraka. Nchi yetu ni ya kidemokrasia na kila raia ana Haki ya kuishi,” ameeleza Rais Samia.

 

 

 

error: Content is protected !!