CHADEMA yasusia vikao vya marekebisho ya sheria

HomeKitaifa

CHADEMA yasusia vikao vya marekebisho ya sheria

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema hakitashiriki katika vikao vya marekebisho ya sheria vinavyoanza leo na kudai kinachopaswa kuanza ni Katiba Mpya. Tume ya Marekebisho ya Sheria inatarajiwa kuanza leo mchakato wa kukusanya maoni ya marekebisho ya sheria.

Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, alisema ni muhimu mchakato huo ukasimamishwa ili kuhakikisha unakwenda kuwa na msaada kwa Watanzania.

“Wasitishe wasisitishe, lakini sisi CHADEMA vikao hivyo vinavyoanza kuanzia kesho “leo” tumeshatoa maelekezo ngazi ya kanda, ili kushusha kwa mkoa na majimbo kutoshiriki vikao hivyo.” alisema na kuongeza:

“Tumefikia uamuzi huo kwa kuzingatia matatizo yetu ya kiuchaguzi msingi wake ni upungufu ulioko kwenye katiba ya sasa,” alisema Mnyika.

Pia, alibainisha upungufu wanaotaka ufanyiwe marekebisho, akidai kuwa katiba ya sasa haijaunda tume huru ya uchaguzi, mfumo mzima wa watumishi wa tume kuanzia mkurugenzi na wasimamizi, na kwamba kikatiba wanapaswa kuwekewa mfumo ambao tume ndiyo itawezesha upatikanaji wao.

 

error: Content is protected !!